Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:37

Japan yaahidi kuipa Ukraine dola za Kimarekani bilioni 4.5 kujiimarisha


Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida

Japan imeahidi kuipa Ukraine dola za Kimarekani bilioni 4.5 kwa ajili ya kuisaidia katika vita vyake dhidi ya Russia, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alitangaza Alhamisi, kati ya fedha hizo dola bilioni 1 zimekusudiwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

“Japan iko imara na inafuata kanuni katika kuisaidia nchi yetu na watu wetu, nashukuru kwa msaada huu,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku Alhamisi. Alisema uamuzi wa Japan kuisaidia Ukraine umekuja “wakati muafaka na wakati unahitajika zaidi.”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Shambulizi la droni ya Russia liliuua mtu mmoja na kuharibu miundombinu ya bandari huko katika mkoa wa Odesa, Ukraine, gavana wa mkoa huo alisema Alhamisi.

Oleh Kiper alisema Odesa ilikuwa ikishambuliwa kwa saa mbili, na wakati mifumo ya ulinzi wa anga iliweza kutungua droni karibuni zote za Russia zilizofanya mashambulizi, baadhi zilipiga katika eneo.

Alimtaja muathirika alikuwa dereva wa lori, alisema shambulizi hilo la droni liliharibu ghala, mashine ya kupandisha vitu na malori karibu na Mto Danube.

Jeshi la Ukraine lilisema shambulizi la anga lililofanywa na Russia lilihusisha jumla ya droni 18 zilizoelekea kupiga Odesa huko kusini mwa Ukraine na mkoa wa Khmelnytskyi katika eneo la magharibi mwa nchi.

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine ilitungua droni 15 kati ya 18, jeshi hilo lilisema.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG