Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:02

Msemaji wa Baraza la Usalama la taifa  White House ataka hatua kuchukuliwa kutoa msaada Ukraine


Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby akizungumza wakati wa mkutano wa kila siku katika Ikulu ya White House huko Washington, Jumatano, Septemba 13, 2023. AP
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby akizungumza wakati wa mkutano wa kila siku katika Ikulu ya White House huko Washington, Jumatano, Septemba 13, 2023. AP

Msemaji wa Baraza la Usalama la taifa  huko White House John Kirby siku ya Ijumaa alitoa wito kwa Bunge la Marekani kuchukua hatua haraka kutoa msaada kwa Ukraine kabla ya mwisho wa mwezi, baada ya hapo itakuwa vigumu kuipatia Kyiv msaada inaohitaji.

Tunahitaji msaada huo mara moja ili tuweze kuwapa usaidizi kwa njia isiyoingiliwa kati, Kirby aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Kirby alisema Marekani inatarajia kwamba Russia itajaribu kuharibu miundombinu muhimu ya nishati ya Ukraine katika msimu huu wa baridi kama ilivyofanya mwaka jana.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema alikutana na makamanda wake wa kijeshi Ijumaa ili kujadili njia za kutoa matokeo madhubuti mwaka ujao katika vita vya nchi hiyo na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG