Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:04

Blinken anasema kuna uungaji mkono mkubwa wa pande mbili kuisaidia Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Jumatano kuna uungaji mkono mkubwa wa pande mbili kwa Ukraine nchini Marekani na hakuna hisia ya uchovu miongoni mwa washirika wa NATO kuendelea na uungaji mkono wao wakati nchi hiyo inaingia katika msimu wa pili wa baridi kali katika vita vyake dhidi ya Russia.

Baadhi wanahoji ikiwa Marekani na washirika wengine wa NATO wanapaswa kuendelea kusimama na Ukraine wakati tunapoingia katika msimu wa pili wa baridi kali wa ukatili wa Putin. Lakini jibu la leo katika NATO lipo wazi, na haliwezi kubadilika. Lazima na tutaendelea kuiunga mkono Ukraine, Blinken alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Brussels siku ya Jumatano.

Tangu vita hivyo vilipoanza, Marekani imetoa kiasi cha dola bilioni 77 za msaada kwenda Ukraine, ambao unajumuisha misaada ya kibinadamu, kifedha na kijeshi, kulingana na Blinken. Alibainisha kuwa washirika wa Ulaya wa Washington wametoa zaidi ya dola bilioni 110 za msaada kwa Kyiv.

Forum

XS
SM
MD
LG