Masoko ya Krismasi, utamaduni unaoenziwa nchini Ujerumani na nchi jirani, yamejiunga katika orodha ndefu ya utamaduni wa kila mwaka ambao umefutwa au umepungua mwaka huu kwa sababu ya janga la virusi vya corona, Shirika la habari la AP linaripoti.
Mwezi Novemba ulishuhudia nchi nyingi za Ulaya zikiweka baadhi ya masharti au katazo kali la kutotoka nje wakati maambukizi mapya ya virusi yakiongezeka.
Masharti hayo ama yanaendelezwa au baadhi yamelegezwa wakati wa kusubiriwa kwa mazao ya Yesu maarufu kama Advent ikianza Jumapili.
Moja ya masoko ya sikukuu yaliyo bora na ya kiasili ni sehemu inayowaleta watalii wengi, yalitangazwa kutofunguliwa mwezi mmoja uliopita.
Masoko nchini kote --- ikiwemo Frankfurt, Dortmund na Berlin --- yameathiriwa na hali hiyo pia, ambapo mamlaka zimesitisha shughuli mbalimbali au waandaaji wakiamua kuwa haiingii akilini kulazimisha mipango yao iendelee.
Kwenye mpaka wa Ufaransa, takriban vibanda 300 vya biashara maarufu ya Krismasi huko Strasbourg havitafunguliwa mwaka huu. Na ni hali hiyo hiyo katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.