Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:40

Mamilioni ya Wamarekani wasafiri licha ya maonyo ya maambukizi ya covid.


Wasafiri wakijiandaa kusafiri katika uwanja wa ndege wa LaGuardia mjini Queens, New York.
Wasafiri wakijiandaa kusafiri katika uwanja wa ndege wa LaGuardia mjini Queens, New York.

Mamilioni ya watu nchini Marekani wanasafiri kabla ya likizo ya siku ya Shukrani, licha ya kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na COVID-19 na rekodi kubwa ya wagonjwa kulazwa hospitalini.

Kudharau huko kwa wasafiri dhidi ya maonyo ya hali inavyozidi kuwa mbaya wakae nyumbani na kupunguza mikusanyiko yao ya likizo hii kunachochea wasiwasi wa wimbi jingine la maambukizo ya virusi vya corona na vifo vya COVID-19 wakati wa msimu wa likizo ya Desemba. kuongezeka kwa kasi katika kesi husababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo baada ya wiki kadhaa.

Wakati watu zaidi walisafiri siku ya Jumanne, idadi ya kila siku ya vifo vya COVID-19 ilizidi 2,000 kwa mara ya kwanza tangu mwezi Mei. Rekodi kubwa ya wagonjwa kulazwa 87,000 iliripotiwa Jumanne wakati Marekani ikirekodi maambukizo mapya milioni 2.3 katika wiki mbili zilizopita pekee.

Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na kuzuia magonjwa na serikali za majimbo na za mitaa zimekuwa zikihimiza sana watu kubaki majumbani na kufanya sherehe zao za Shukrani kuwa ndogo.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington Dc

XS
SM
MD
LG