Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:09

WHO yaitaka Afrika kujiandaa na usambazaji wa chanjo ya corona


Mtu aliyejitolea kupewa chanjo ya majaribio ya covid 19 akipewa chanjo hiyo katika hospitali ya Chris Hani Baragwanath Soweto, Johannesburg, Afrika Kusini Juni 24, 2020.
Mtu aliyejitolea kupewa chanjo ya majaribio ya covid 19 akipewa chanjo hiyo katika hospitali ya Chris Hani Baragwanath Soweto, Johannesburg, Afrika Kusini Juni 24, 2020.

Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington Dc

XS
SM
MD
LG