Baraza hilo likiachana na majuma kadhaa ya kutochukua hatua na mabishano, hasusani kwa ajili ya ulinzi wa watoto, lakini Israel haraka imekataa hatua hiyo.
"Rasimu hii ya azimio tuliyonayo mbele yetu hivi leo inataka kutoa matumaini katika muda huu wenye giza," Balozi wa Malta Vanessa Frazier, ambaye aliongoza mazungumzo na kuandaa waraka huo.
"Inalenga kuhakikisha utulivu kutokana na jinamizi la sasa huko Gaza na kutoa matumaini kwa familia za waathirika wote. Hasa inaangazia masaibu ya watoto waliokwama katika eneo la vita na wale wanaoshikiliwa mateka."
Azimio hilo linataka "kuongeza sitisho la muda kwa masuala ya kibinadamu na njia za ufikishaji misaada huko Gaza "kwa siku kadhaa za kutosha" kuruhusu misaada kuingia, kurekebisha uharibifu wa miundombinu muhimu kama vile hospitali, visima vya maji na maduka ya kuokea mikate, na kuwezesha uokoaji wa kitabibu, hususani kwa watoto.
Pia inataka "kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote" wanaoshikiliwa na Hamas na makundi mengine – hususani watoto.
Maazimio ya baraza yana nguvu ya kisheria, lakini wahusika waliotajwa mara kwa mara huyapuuza, na kusababisha mafanikio kidogo.
Ujumbe kutoka Israel aliliambia baraza hilo kwamba serikali yake haihitaji azimio la kuikumbusha kuzingatia sheria za kimataifa na kwamba Hamas "haitajisumbua kuisoma.
"Kwa hivyo, azimio hili halisaidii chochote katika kuchangia hali iliyopo," naibu mjumbe wa Israeli Brett Jonathan Miller alisema.
"Kurejeshwa kwa mateka wetu nyumbani ni kipaumbele cha juu cha Israeli, na kuona kwamba maazimio ya Baraza la Usalama hayana uhusiano wowote na magaidi, Israeli itaendelea kufanya chochote kinachohitajika ili kufikia lengo hili."
Forum