Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:34

Chuki dhidi ya Wayahudi na Waislamu zaongezeka Australia


Wanachama wa jumuiya ya Wayahudi huko Australia wakiwa katika maandamano yaliyofanyika Sydney Novemba 12, 2023. Picha na DAVID GRAY / AFP.
Wanachama wa jumuiya ya Wayahudi huko Australia wakiwa katika maandamano yaliyofanyika Sydney Novemba 12, 2023. Picha na DAVID GRAY / AFP.

Wabunge wa Kiyahudi nchini Australia wanasema chuki dhidi ya Wayahudi katika taifa hilo zimeongezeka, wakati vita huko Gaza vimeshika kasi.

Wakati huo huo, viongozi wa Kiislamu wanasema kuwa chuki dhidi ya Uislamu zimeongezeka.

Wakati Australia inajivunia kuwa moja ya mataifa yenye tamaduni nyingi sana duniani, vita kati ya Israel na Hamas vimezua msuguano.

Islamophobia Register Australia, ambayo inaorodhesha uhalifu wa chuki, mwezi uliopita imebainisha matokeo 133, lakini taasisi ya kijamii imeviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa idadi sahihi ilikuwa "juu zaidi" kwa sababu manyanyaso mengi hayaripotiwi.

Baraza Kuu la Utendaji la Australian Jewry limeorodhesha matukio 221 ya chuki za kidini kati ya Oktoba 8 na Novemba 7. Kuanzia Oktoba 1 hadi Oktoba 7, tarehe ya shambulio la Hamas, kulikuwa na tukio moja.

Unyanyasaji huo unajumuisha vitisho ghasia za bunduki, vitisho kwenye misikiti na masinagogi pamoja na kwenye shule za Waislamu na Wayahudi, ikiwemo uharibifu wa mali na matusi. Mashambulio ya kimwili pia yameripotiwa.

Mjini Canberra, wabunge Wayahudi wamesema matukio ya chuki za kidini "hazikuwa zimeelezewa" nchini Australia.

Kumekuwepo na maandamano makubwa ya kuwaunga mkono Wapalestina nchini Australia katika wiki za hivi karibuni, pamoja na maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG