Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 05:31

Jeshi la Israel lasambaza video za chumba cha hospitali inachodai Hamas inahifadhi silaha


Magari ya kijeshi ya Israel yakiwa katika operesheni ya ardhini inayoendelea dhidi ya Hamas Novemba 12, 2023. Picha na Reuters
Magari ya kijeshi ya Israel yakiwa katika operesheni ya ardhini inayoendelea dhidi ya Hamas Novemba 12, 2023. Picha na Reuters

Jeshi la Israel limesambaza video na picha siku ya Jumatatu zikionyesha kile ilichosema ni silaha zilizohifadhiwa na Hamas katika chumba cha chini cha hospitali ya watoto huko Gaza ambako pia lilisema kuwa ilionekana kuwa mateka walishikiliwa huko.

Msemaji wa Jeshi la Israel Admiral Daniel Hagari alisema kuwa wanajeshi wamegundua kituo kikuu chenye silaha pamoja na maguruneti, fulana zakujitoa mhanga na vilipuzi vingine vilivyohifadhiwa na wapiganaji wa Hamas katika eneo la chini la Hospitali ya Rantissi, ambayo ni hospitali ya watoto inayotibu wagonjwa wa saratani.

"Na pia tulipata ishara zinazoonyesha kuwa Hamas ilikuwa ikiwashikilia mateka hapa," alitoa maelezo hayo kwa njia ya televisheni. "Hili kwa sasa tunalichunguza. Lakini pia tuna taarifa za kijasusi zinazothibitisha hilo."

Aidha, wanajeshi walipata pikipiki yenye alama za risasi ambayo alisema ilionekana ilitumiwa kuwaleta mateka Gaza baada ya shambulio la ghafla la Oktoba 7 wakati wapiganaji wa Hamas walipovamia kusini mwa Israel, na kuua takriban watu 1,200 na kuwakamata mateka wapatao 240, kulingana na mamlaka za Israeli.

Katika kulipiza kisasi, Israel imeanzisha mashambulizi makali ya mabomu huko Ukanda wa Gaza na kufuatiwa na operesheni ya ardhini ambayo imeshuhudia wanajeshi wakiingia ndani kabisa ya eneo hilo. Zaidi ya watu 11,000 wameuawa huko Gaza, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.

Siku ya Jumatatu, vifaru vya Israel viliwekwa nje ya milango ya hospitali ya Shifa, hospitali kuu ya Gaza ambako mamia ya wagonjwa walikuwa bado wanasubiri kuhamishwa.

Forum

XS
SM
MD
LG