Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 01:26

Iraq: Eneo lenye ulinzi mkali Baghdad, Green Zone lashambuliwa


Wabunge wa Iraqi wakihudhuria kikao cha kumchagua Rais mpya wa Iraq mjini Baghdad.

Jeshi la Iraq limesema Alhamisi roketi tisa zimetua katika eneo lenye ulinzi mkali la Green Zone mjini Baghdad.

Shambulizi limetokea wakati wabunge wakikusanyika kwa ajili ya kikao cha bunge kumchagua rais mpya.

Maafisa wa usalama walisema takriban watu watano walijeruhiwa.

Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na shambulizi hilo.

Makombora yalirushwa kulenga eneo la Green Zone mwishoni mwa mwezi uliopita wakati wabunge walipokuwa wakikutana kupiga kura kumchagua spika wa bunge.

Some information for this report came from The Associated Press, Agence France-Presse and Reuters.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG