Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:15

Kiongozi wa Kishia Moqtada al-Sadr asema anaachana na siasa na kufunga taasisi zake

Wafuasi wa kiongozi wa Iraq Moqtada al-Sadr wakusanyika kwa sala ya Ijumaa nje ya bunge, huko Baghdad. Agosti 26, 2022. REUTERS/Alaa Al-Marjani.
Wafuasi wa kiongozi wa Iraq Moqtada al-Sadr wakusanyika kwa sala ya Ijumaa nje ya bunge, huko Baghdad. Agosti 26, 2022. REUTERS/Alaa Al-Marjani.

Kiongozi mwenye nguvu wa dhehebu la kislamu la shia Moqtada al-Sadr amesema Jumatatu  kwamba anaachana na siasa na kufunga taasisi zake ikiwa ni mwitikio wa mwendendo usio mzuri wa kisiasa, ambapo hatua yake hiyo inaweza kuchochea ukosefu wa  uthabiti.

Katika taarifa aliyoitoa katika ujumbe wa Twitter, akiwakosoa viongozi wenzake wa kishia kwa kutounga mkono mwito wake wa mabadiliko, alitangaza kwamba kwa sasa anajitoa na masuala hayo ya kisiasa.

Hakuweka wazi kuhusu kufunga ofisi yake lakini amesema taasisi za kitamaduni na kidini zitaendelea kufanya kazi.

Sadr huko nyuma amewahi kutoa tangazo kama hilo licha ya kwamba hali ya sasa ya kisiasa inaonekana kuwa ngumu kukabiliana nayo ikilinganishwa na kipindi cha nyuma. Mvutano wa sasa baina ya Sadr na wapinzani wake wa kishia imeifanya Iraq kutokuwa na serekali kwa kipindi kirefu.

XS
SM
MD
LG