Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:08

Mamia ya waandamanaji wavamia jengo la bunge la Iraq.


Waandamanaji wa Iraq
Waandamanaji wa Iraq

Mamia ya wafuasi wa kiongozi wa kidini Muqtada al-Sadr waliingia katika jengo la bunge jumamosi kwa mara ya pili wiki hii.

Mamia ya wafuasi wa kiongozi wa kidini Muqtada al-Sadr waliingia katika jengo la bunge Jumamosi kwa mara ya pili wiki hii.

Mapema, vikosi vya usalama vya Iraq vilipambana na maelfu ya waandamanaji katika mji wa Baghdadkwenye eneo linalojulikana kama Green zone.

Waandamanaji walitumia Kamba kuvuta vizuizi vilivyoundwa kwa sementi ili waweze kufikia lango kuu la Green zone ambako majengo ya ofisi na balozi za kigeni vipo.

Polisi wa Iraq walitumia gesi ya machozi na mabomu yenye sauti kubwa kutawanya waandamanaji wakati walipokuwa wanasogea katika jengo la bunge.

Waandishi wa shirika la habari la AP walishuhudia polisi kadhaa wakiwa wamejeruhiwa.

Al- Sard aliitisha maandamano kupinga kuunda serikali mpya inayoungwa mkono na makundi ya kisiasa ya Iran wakati kipindi cha bunge la kawaida kikitarajiwa kuanza.

Chama cha Al- Sadr kiliondoka katika mazungumzo ya kuunda serikali mwezi Juni na kuruhusu wapinzani wake katika kamati ya uratibu kufikia wingi unaohitajika kuendelea na utaratibu.

XS
SM
MD
LG