Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 06:20

IEBC yatangaza kurudiwa uchaguzi wa urais Kenya Octoba 17


Wafula Chebukati wa IEBC

Uchaguzi wa urais nchini Kenya utarudiwa Octoba 17, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ametangaza Jumatatu.

Katika tamko lake, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati amesema hakutakuwa na uteuzi mpya katika uchaguzi huu.

Chebukati amesema Kiongozi wa NASA peke yake Raila Odinga, na Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na wagombea wenza wao watashiriki.

Mgombea mwenza wa Odinga ni Kalonzo Musyoka na yule wa Kenyatta ni makamu wake William Ruto.

“Tume hiyo inapitia taratibu na hatua zinazohitajika kuendesha uchaguzi huo upya na itawajulisha wadau wote mapema baadae,” amesema

Kufuatia tangazo hilo la IEBC, Dkt Ekuru Aukot wa Chama cha Thirdway Alliance, ambaye alikuwa mgombea urais katika uchaguzi Agosti 8, amesema uamuzi huo kuwazuia wagombea wengine kurudia kinyang’anyiro hicho ni kinyume cha sheria na ni batili.”

Katika ujumbe wake wa Twitter Dr Aukot amesema; “ Tunaelekea Mahakamani kudai haki yetu.”

Mahakama ya Juu inayoongozwa na Jaji Mkuu David Maraga Septemba 1 ilitangaza kubalitisha kwa uchaguzi wa Agosti 8 nchini Kenya kutokana na uchaguzi huo kukiuka katiba na sheria za uchaguzi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG