Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:30

IEBC yatoa angalizo juu ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi


Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Tume ya Uchaguzi imetangaza jinsi watu watavyoweza kupata matokeo ya uchaguzi Agosti 8, wakati wa Uchaguzi Mkuu Kenya.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumanne imesema kuwa matokeo ya uchaguzi yatatolewa kupitia vyombo vya habari na tovuti ya tume.

Mkuu wa Tume Ezra Chiloba amewahakikishia viongozi wa vyombo vya habari vya kigeni, wahariri, wazalishaji wa vipindi na timu za wataalamu kupata habari za uchaguzi kutoka katika kituo cha kutangaza kura cha Taifa Nairobi.

“Matokeo yatatangazwa kwa kuzingatia matokeo halisi kutoka katika vituo vya kupiga kura,” amesema alipokutana na wadau wa vyombo vya habari katika ofisi za Bomas huko Nairobi.

“Hatutarajii kuwa na tofauti kati ya fomu za matokeo kwenye vituo vya kupiga kura na takwimu zinazotolewa kielektroniki.

Amesema tume haitotangaza matokeo ya jimbo lolote katika kituo chake cha kitaifa cha kujumlisha matokeo ya uchaguzi, akimaanisha kuwa maafisa wa uchaguzi kwenye vituo vya kupiga kura watakuwa na kauli ya mwisho.

“Hatujui itachukua muda gani kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa,” amesema.

Kwa kuwa maafisa uchaguzi hawatotakiwa kusafiri kuja Nairobi zoezi hilo litakuwa la haraka.”

Kwa mujibu wa Mkuu wa tume, hailazimiki kwa wasimamizi wa uchaguzi makao makuu Nairobi kusafiri mpaka kwenye vituo vya kujumlisha matokeo katika majimbo kwa sababu matokeo yanaweza kutumwa kieletronikia.

Inamaanisha kuwa matokeo yatapelekwa kwanza katika vituo vya kujumuisha kura, ilikuzuia uwezekano wowote wa matatizo ya kimitandao.

Jumla ya vituo 338 vya kupiga kura vimewekewa mawasiliano ya internet nchi nzima, amesema kwa ajili ya uchaguzi.

Amesema mfumo wa usimamizi wa pamoja wa uchaguzi Kenya (KIEMS) ambao utatumiwa na tume utafanya iwe vigumu kabisa kura kuchakachuliwa au kuibiwa.

XS
SM
MD
LG