Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:55

Somalia yasema idadi ya walioathirika Mogadishu inaweza kuongezeka


Wanajeshi wa Somalia wakiwaondowa walojeruhiwa katika shambulio baya la Mogadishu, Oct 14, 2017
Wanajeshi wa Somalia wakiwaondowa walojeruhiwa katika shambulio baya la Mogadishu, Oct 14, 2017

Idadi ya wahanga wa mlipuko wa bomu uliyotokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu umefikia watu 300.

Wakati huohuo timu za waokoaji zinaendelea kutafuta watu waliokuwa wamenusurika kutokana na mlipuko mkubwa uliofungamanishwa na wapiganaji wa Kiislam.

Dr Abdulkadir Adam, Mkuu wa huduma za magari ya wagonjwa Mogadishu, ameiambia VOA kuwa watu 302 wamethibishwa kuuwawa kutokana na mlipuko huo, ambao ulilenga eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara katika mji Mkuu wa Somalia Jumamosi jioni.

Serikali imesema kuwa watu 429 walijeruhiwa na wamepelekwa katika mahospitali nchini humo, na inawezekana idadi ya vifo ikaongezeka. Zaidi ya watu 30 waliokuwa wameumia vibaya sana wamesafirishwa kupelekwa Uturuki Jumatatu kwa matibabu, akiwemo Mwandishi wa VOA Abdulkadir Mohamed Abdulle.

Mpaka hivi sasa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulizi hilo lakini maafisa wa serikali ya Somalia na wataalamu wa masuala ya ugaidi wanaamini kuwa kikundi cha al-Shabab kilikuwa kimeendesha shambulizi hili.

“Iwapo watadai kuhusika au watakataa haitabadillisha kitu chochote, sisi tunafahamu kuwa kitendo kilichotokea ni cha al-Shabab,” aliyekuwa afisa wa Usalama Abdi Hassan ameiambia VOA. Taarifa zinazotufikia ni kwamba hii ni kazi ya al-shabab, na kitendo hiki ndiyo ishara yenyewe.

Hata hivyo kikundi hicho kimekaa kimya tangu mlipuko huo utokee, lakini wameuwa mamia ya watu katika miaka ya karibuni kupitia mashambulizi waliofanya katika mahoteli, migahawa na maeneo ya umma mjini Mogadishu.

Vyanzo vya habari nchini Somalia vimesema kuwa familia nchini Somalia zimeanza kuwazika wapendwa wao mjini Mogadishu kufuatia mlipuko huo.

Baadhi ya familia huwenda wasiweze kuwaona wapendwa wao kwa sababu waathirika wengi waliungua vibaya na kushindwa kutambulika.

Meya wa Mogadishu, tabis Abdi Mohamed alisema hakuna kitu kibaya pale mtu anapotoka kuona maiti na anashindwa kumtambua mpendwa wake. Aliendelea kusema kuwa shambulizi hili halielezeki.

Naye mwanaharakati Abubakar Shekf alisema kila nyumba watu wanalia. Serikali ilisema katika taarifa yake kwamba imeweka kituo cha dharura katika mji mkuu ili kusaidia kuziunganisha familia.

XS
SM
MD
LG