Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 18:25

Idadi ya vifo katika vita vya Sudan yafikia zaidi ya watu 600


FILE PHOTO: Picha za Satellite zinaonyesha Kituo Kikuu cha Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Sudan kikiwa kimeharibiwa mjini Khartoum.

Shirika la Afya Duniani limesema idadi ya vifo kutokana na vita vibaya vya takriban mwezi mmoja nchini Sudan sasa ni zaidi ya watu 600.

WHO imesema Jumanne kwamba zaidi ya watu 5, 000 wamejeruhiwa kutokana na mapigano hayo baina ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yameshindwa kumaliza mzozo au hata kufanya ili kupunguza ghasia .

Umoja wa Mataifa umesema mlipuko wa mapigano Sudan unataabisha hali ya kibinadamu Abyei katika mpaka wa Sudan Kusini na Sudan.

Hanna Serwaa Tetteh , mwakilishi wa umoja wa mataifa katika umoja wa Afrika anaeleza: “Wakati mamlaka za Sudan hivi sasa haziko katika nafasi ya kulinda mipaka yake hali ya ukosefu wa usalama mpakani baina yaSsudan na Sudan Kusini inaweza kuongezeka wakati wa harakati za kuvuka mpaka kwa makundi yenye silaha na ya uhalifu."

Ameongeza kuwa: "Mapigano nchini Ssudan pia yanaathiri shughuli za kibiashara za kila siku na usambazaji wa chakula na bidhaa nyingine muhimu kutoka Sudan kwenda Sudan Kusini na kuhatarisha uuzaji wa mafuta kutoka kusini.”

Wajumbe wa pande zote mbili wamekuwa wakikutana mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa siku kadhaa kwa lengo la kufikia makubaliano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya watu wenye shida ya chakula, makazi, huduma za afya mjini Khartoum na miji mingine ya Sudan.

Saudia Arabia tayari imeahidi kwamba itaipa Sudan misaada yenye thamani ya dola milioni 100.

XS
SM
MD
LG