Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Usafirishaji bidhaa wasimama katika mji wa Port Sudan


Wafanyakazi wakipakua mizigo kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) na msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Port Sudan, mji wa Port Sudan
Wafanyakazi wakipakua mizigo kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) na msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Port Sudan, mji wa Port Sudan

Magari makubwa yaliyojaa bidhaa yamekwama katika mji wa Port Sudan yakishindwa kusafiri huku kukiwa na mapigano baina ya pande mbili hasimu mjini Khartoum.

Wakati bandari imekuwa ndiyo njia kubwa kupitia Sudan magari makubwa yaliyosimama yaliashiria kuwa mzozo mkubwa unakuja.

Pande mbili zinazogombana nchini Sudan zilianza mazungumzo Jumamosi yenye lengo la kuimarisha sitisho la mapigano lililoshindwa baada ya wiki tatu za mapigano ambayo yameuwa mamia ya watu.

Taarifa chache zimetolewa kwa umma kuhusu mazungumzo hayo yanayoongozwa na Saudi Arabia na Marekani mjini Jeddah kati ya jeshi la Sudan SAF na kikosi cha RSF yaliyoanza Mei 6.

Lakini kiongozi wa SAF Jenerali Abdel Fattah al Burhan Jumatatu alikiambia kituo cha televisheni cha Misri –Al-Qahera News TV, kwamba hakuna umuhimu wa kuketi pamoja kwenye meza ya mashauriano nchini Saudi Arabia bila ya kuwa na sitisho la mapigano la kweli.

Jenerali Burhan amesema anakaribisha juhudi zote zenye lengo la kusitisha umwagaji damu lakini akasisitiza kwamba RSF lazima iweke silaha zake chini.

​
XS
SM
MD
LG