Hillary Clinton ameweka historia licha ya changamoto za kisiasa na kibinafsi na kua mwanamke wa kwanza kushinda uteuzi wa chama kikuu cha kisiasa Marekani. Akishinda uchaguzi wa Novemba atakua mtu wa kwanza kua mke wa rais, Seneta wa New York waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje na kua Bibi Rais.
Maisha ya Hillary Clinton katika picha

1
Hillary Rodham alizaliwa October 26, 1947. alikulia katika mtaa wa watu wa tabaka la wastani huko Park Ridge, Illinois, kiunga cha Chicago. (hillaryclinton.com)

2
Babake Hugh, alikua shujaa wa vita vya pili duniani katika jeshi la majini na Mrepublican maisha yake yote. katika picha na mamake na kakake zake, Hugh Jr. na Anthony. (hillaryclinton.com)

3
Hillary alikutana na Bill Clinton alipokua anasoma chuo kikuu cha Yale. walianza kua pamoja tangu 1971. (hillaryclinton.com)

4
Baada ya kuhetimu uwanasheria, Hillary alifanya kazi na Fuko la kutetea watoto, Children’s Defense Fund. (hillaryclinton.com)