Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 09:18

Hasina ashinda awamu ya tatu Bangladesh


Waziri Mkuu Sheikh Hasina alipokuwa akipiga kura wakati wa uchaguzi mkuu mjini Dhaka, Bangladesh, Disemba 30, 2018

Maafisa wa uchaguzi nchini Bangladesh wametangaza kwamba muungano wa vyama vya kisiasa unaoongozwa na Waziri Mkuu Sheikh Hasina, umeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi kubwa ya wabunge.

Ushindi wa Hasina, unampa fursa ya kutawala kwa mhula wa tatu mfululizo japo washindani wake wamekataa matokeo.

Muungano wa vyama vya kisiasa wa Awami, umepata viti vya bunge 288 kati ya 300.

Muungano wa upinzani, ukiongozwa na Kamal Hossain umepata viti sita.

Hossain ametaja uchaguzi huo wa Jumapili kuwa ulahgai, na ambao matokeo yake yatakataliwa, akisema wapiga kura walitishiwa, huku udanganyifu katika hesabu ya kura ukifanyika.

Machafuko yameripotiwa wakati wa kampeni licha ya kuwepo idadi kubwa ya maafisa wa usalama.Mohammad Rabiul, ni mpiga kura.

"matokeo ya vurugu ni kawaida wakati wa uchaguzi. Kwa mtazamo wako, uchaguzi ulikuwa huru na haki na iwapo wanasiasa wa upinzani hawakupata matokeo waliotarajia, watalalamika, ilivyo kawaida. "

Watu 13 waliuawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na wale wa chama kinachotawala huku wanaumme watatu wakipigwa risasi na polisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG