Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:32

Watu 17 wameuwawa katika uchaguzi Bangladesh


Uchaguzi nchini Bangladesh
Uchaguzi nchini Bangladesh

Matokeo ya awali yalionesha chama cha Awami League cha Waziri Mkuu Sheikh Hasina kinaelekea kupata ushindi lakini kiongozi wa ushirika wa upinzani Kamal Hossain aliuita uchaguzi wa Jumapili uliojaa ujinga na alisema matokeo yatakataliwa.

Watu takribani 17 wameuwawa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi nchini Bangladesh siku ya Jumapili kwa mujibu wa polisi wakati Sheikh Hasina alipokuwa anaongoza kwa idadi kubwa ya kura na kushinda muhula wa tatu kama Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina akionesha vidole baada ya kupiga kura
Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina akionesha vidole baada ya kupiga kura

Matokeo ya awali ya uchaguzi yalionesha chama cha Awami League cha Waziri Mkuu Hasina kinaelekea kupata ushindi. Lakini wapinzani wanakosoa ripoti za manyanyaso kwa wapiga kura na kasoro nyingine katika uchaguzi. Kiongozi wa ushirika wa upinzani Kamal Hossain aliuita uchaguzi wa Jumapili uliojaa ujinga na alisema matokeo yatakataliwa.

Ghasia kati ya chama tawala na vyama ya upinzani ambazo zilivuruga kampeni za uchaguzi ziliendelea hadi siku ya uchaguzi licha ya usalama mkali kuwepo nchi nzima ikiwemo wanajeshi 600,000 na vikosi vingine vya usalama vilivyowekwa nchi nzima kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa.

Wapigakura waliojitokeza katika nchi yenye watu milioni 165 walikuwa wachache katika uchaguzi mkuu wa kwanza uliokuwa na ushindani mkali katika kipindi cha muongo mmoja.

XS
SM
MD
LG