Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:38

Uhuru wa vyombo vya habari unaendelea kubanwa Afrika


FILE - Waandishi habari na wanaharakati waandamana siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani May 3, 2018, mjini Nakuru, Kenya.
FILE - Waandishi habari na wanaharakati waandamana siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani May 3, 2018, mjini Nakuru, Kenya.

Kila mwaka Mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari inayoadhimishwa kote duniani lakini kutokana na janga la Corona mwaka huu siku hii inaadhimishwa kupitia vyombo vya habari na mitandao, bila sherehe maalum za kawaida, kuhamasisha haki na uhuru wa waandishi na vyombo vya habari. 

Kihistoria siku ya uhuru wa vyombo vya habari iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba 1993 kutokana na ushauri wa shirika la elimu na sayansi la umoja huy, UNESCO.

Iliamuliwa tarehe 3 Mei sherehe hizo zifanyike ili pia kuadhimisha "Tangazo la Windhoek," juu ya uhuru wa vyombo vya habari barani Afrika, na kujulikana sasa kama Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Uandishi wa Habari bila ya Uoga au Upendeleo." Na katika ujumbe wake siku ya Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, amesema wakati janga la COVID 19 likiendelea, limetoa pia fursa kwa janga la pilli nalo ni habari za upotoshaji kutokana na ushauri wa hatari wa afya unaotokana na nadharia za dhana zisizo na msingi.

Hivyo anasema, vyombo vya habari ni muhimu kuripoti juu ya habari zilizothbitishwa, kwa msingi wa habari zenye ukweli wa kisayansi na uchambuzi.

Wakati huo huo taasisi mbali mbali za dunia hutoa takwimu na orodha ya hali ya waandishi wa habari katika takriban mataifa 180 ya dunia na Norway inaongoza kwa kuwa na uhuru mkubwa wa wandishi habari, na Korea kaskazini nchi ya mwisho kulingana na takwimu za Freedom House hapa Marekani.

Ethopia inatajwa kama nchi iliyofanya mageuzi makubwa na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari barani Afrika tangu kuingia madarakani Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Nayo Eritrea ndio nchi ya mwisho barani humo ikiwa pia ni ya tatu kutoka chini duniani yenye kukandamiza uhuru wa waandishi habari.

Huko Afrika masharki, Kenya ambayo iko nafasi ya 103 katika orodha ya nchi zenye uhuru wa vyombo vya habari duniani baadhi ya mashirika ya habari yanawapunguzia mishahara waandishi habari, wengine wakifutwa kazi huku wanahabari wengine wakieleza kutoridhikia mazingira wanamofanyia kazi hususan kutokana na manyanyaso kutoka kwa asasi za usalama na umma kwa ujumla.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Kenya 2020
please wait

No media source currently available

0:00 0:07:12 0:00

Tanzania yaendelea kubana uhuru wa vyombo vya Habari
Kwa upande wake Tanzania bado inachangamoto za kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe na wadau wakiendelea kusema kuwa hali hiyo ya ukandamizaji inaendelea kuongezeka.

Pia matukio ya vyombo vya habari kutumbukia katika mikono ya dola yakielezwa kuwa makubwa.

Kumekuwa na mlolongo wa matukio ya vyombo vya habari kupewa adhabu au kufungiwa ama kupigwa faini na kile ambacho mamlaka za kiutendaji ikisema kwamba kukiukwa kwa sharia.

ingawa baadhi ya sheria hizo ikiwemo ile ya huduma kwa vyombo vya habari ya mwaka 2016 na nyinginezo kupigiwa kelele na kuwepo baadhi ya vipengele vinavyo minya uhuru wa maoni bado sheria hizo zimeendelea kutumiwa.

Watetezi wa uhuru wa maoni pamoja na haki za binadamu wanasema kwamba mazingira ya wanahabari ya kufanya shughuli zao yanakabiliwa na wakati mgumu kuliko nyakati nyingine.

Katika ripoti yake mpya ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu unataja madhila mbalimbali ambayo vyombo vya habari na waandishi wake kwa ujumla wamekuwa wakipitia ikiwemo yale ya kutiwa mbaroni na wakati mwingine kuzuiwa kufanya kazi zao.

Kufuatana na afisa wa mtandao huo misukosuko inaendelea kuwakumba watetezi wa haki za binadamu inakaribiana na ile inayowakabili waandishi wahabari.

Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka (RSF) linaitaja Tanzania kama nchi ambayo waandishi wa habari wanapitia katika wakati mgumu. Mmoja ya hayo ni kupotea kwa mwandishi wa habari wa kujtegemea Azory Gwanda jambo linaloendelea kuakisi matokeo ya jumla yanayowaandama waandishi wa habari, ingawa serikali imekuwa ikikanusha kuwabana wanahabari.

Baraza la Habari Tanzania (MCT) linasema mazingira yanayoendelea kuwabana waandishi wa habari wanapokuwa katika majukumu yao hayakubaliki na yanapaswa kukemewa kwa kauli zote.

Matumizi mabaya ya madaraka upindishwaji wa sheria, unyanyasaji na ujahili na hata matamshiya vitisho kutoka kwa viongozi kwa wanahabari na vyombo vyao yakiambatana na ari kubwa ya kufungia vyombo vya habari kwa kiasi ambacho hakijawahi kuonekana katika historia ya Tanzania ni mambo ambayo yanalishushia hadhi taifa letu mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Uhuru wa vyombo vya habari unakandamizwa Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:47 0:00

Wanahabari wanyanyaswa Uganda

Nchini Uganda matokeo ya waandishi wa Habari kuchapwa, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka yanatajwa kuwa yanalengo la kuwatisha kufanya kazi yao, matukio hayo na yameendelea kuripotiwa.

Viongozi serikali wanaendelea kuweka masharti na kupitisha sheria zinazo onekana kubana uhuru wa vyombo vya habari huku tume ya kusimamia mawasiliano nchini humo ikishutumiwa kwa kuwa msitari wa mbele katika kuminya uhuru wa Habari.

Waandishi habari waendelea kunyanaswa na vyombo vya usalama Uganda
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:52 0:00

Vyombo vya habari vya DRC havina uwezo wa fedha

Na katika jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uwezo wa kuripoti na vyombo vya habari kutokuwa na fedha za kutosha kugharimia kazi zao.

Vyombo vya habari vina kabiliwa na changamoto kugharimia kazi zao DRC
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:00 0:00

Imetayarishwa na Waandishi wetu, Washington DC, Kenya, Uganda na DRC,

XS
SM
MD
LG