Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 07:53

Gbagbo atowa wito wa kusitishwa uhasama Ivory Coast


Wapiganaji wa rais mteule wa Ivory Coast Alassane Ouattara wakipiga doria katika mji wa Abidjan, Aprili 10, 2011
Wapiganaji wa rais mteule wa Ivory Coast Alassane Ouattara wakipiga doria katika mji wa Abidjan, Aprili 10, 2011

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ametoa wito wa kusitishwa mapigano baada ya kukamatwa Jumatatu na wapiganaji wa Alassane Outtara.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo ametowa wito kwa wafuasi wake kuweka chini silaha ili kumaliza mgogoro wa kisiasa na kurejesha maisha katika hali ya kawaida

Bw. Gbagbo amesema “mapigano yameisha”, na ndio maana amemuomba mkuu wake wa utawala kutoka nje na “kupeperusha kitambaa cheupe” ambayo ni ishara ya kumaliza mapambano.

Bw. Gbagbo alizungumza katika televisheni inayosimamiwa na rais mteule Alassane Ouattara, masaa machache baada ya kukamatwa na wapiganaji wa Bw. Ouattara siku ya Jumatatu.

Majeshi ya Ufaransa yalizingira makazi ya Bw. Gbagbo, lakini yamesema kuwa hawakuingia ndani ya handaki ambalo wapiganaji wa Bw. Ouattara walimkamata rais huyo wa zamani,na wakampa vazi la kuzuia risasi, kofia ya chuma na kisha kuwaweka kizuizini pamoja na mkewe na mwanae.

Bw. Gbagbo anashikiliwa katika hoteli ambayo ni makao makuu ya Bw. Ouattara, mahali ambapo Bw. Ouattara alilihutubia taifa katika kile alichokiita “siku ya kihistoria”.

Bw. Ouattara anasema “ukurasa mweupe umefunguka kwa watu wa Ivory Coast, mweupe kama rangi nyeupe iliyopo kwenye bendera ya taifa ambayo inawakilisha matumaini na amani”. “Kwa pamoja raia wa Ivory Coast wanaweza kuandika hadithi yao ya kusameheana na maridhiano”

Bw. Ouattara amehakikisha usalama wa Bw. Gbagbo na kuwahakikishia watu wa Ivory Coast kwamba rais huyo wa zamani atafikishwa mbele ya mahakama.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa Bw. Gbagbo hastahili kupewa hifadhi na nchi yoyote ya nje ambayo itamkinga na mashitaka.

Wakati huo huo, kundi hilo limesema kwamba majeshi ya Bw. Ouattara yana wajibu wa kutekeleza sheria za kimataifa kwa kutumia utu wakati wote watakapomshikilia Bw. Gbgbo pamoja na washirika wake.

Kukamatwa kwa Bw Gbagbo kumemaliza miezi minne ya mvutano wa kisiasa baina ya wapinzani hao wa urais wakati majeshi ya Gbagbo yalipoanza kumkimbia taratibu kiongozi wao.

Mamia ya wanjaeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais Republican Guard walijisalimisha kwa walinda usalama wa Umoja wa Mataifa jana. Bw. Ouattara baadae alikutana na baadhi ya majenerali wa zamani wa jeshi la Gbagbo.

Kufuatia kukamatwa kwa Bw. Gbagbo, msemaji wa afisi ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Hamadoun Toure, amesema kwamba kazi inayopewa kipaumbele hivi sasa ni kurejesha sheria na utaratibu jijini Abidjan, hasa kwa kuwa wafuasi wengi wa tawi la wanamgambo vijana la Bw. Gbagbo wako mitaani baado.

XS
SM
MD
LG