Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:21

Mapigano yaendelea Ivory Coast


Wanajeshi wanaomuunga mkono Gbagbo wakifanya doria kwenye mitaa karibu na makazi ya Rais mjini Abidjan, April 3, 2011
Wanajeshi wanaomuunga mkono Gbagbo wakifanya doria kwenye mitaa karibu na makazi ya Rais mjini Abidjan, April 3, 2011

Mitaa ya mjini Abidjan haina watu, huku wakazi wakiendelea kukabiliana na mapigano ya mwisho kati ya majeshi ya marais wawili wapinzani nchini Ivory Coast.

Hakuna ripoti yeyote juu ya mapigano ya leo Jumatatu, lakini mashahidi wanasema watu wengi wamebaki majumbani mwao, na wanatoka nje kwa ajili ya kununua chakula tu.

Majeshi yanayomuunga mkono Rais anayetambuliwa kimataifa Alassane Ouattara waliteka sehemu kubwa ya nchi wiki iliyopita, na hivi sasa wanaonekana wanajaribu kumuangusha Rais Laurent Gbagbo anayeng’ang’ania madaraka.

Waziri Mkuu wa bwana Ouattara, Guillaume Soro alisema leo Jumatatu kwamba hali imeongezeka kwa ajili ya mashambulizi ya haraka.

Hata hivyo bwana Gbagbo bado ana kundi la wanajeshi wanaomtii ambao wamezunguka makazi ya Rais mjini Abidjan, mahali anapoishi.

Alipata nguvu Jumapili jioni wakati mkuu wake wa utawala katika jeshi, jenerali Phillippe Mangou, alipoondoka nyumbani kwa balozi wa Afrika Kusini baada ya kuomba hifadhi pamoja na familia yake wiki iliyopita. Kuna taarifa kwamba Mangou amerudi tena kwenye kazi yake katika jeshi.

Bwana Ouattara alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba, lakini bwana Gbagbo anakataa kuachia madaraka.

XS
SM
MD
LG