Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:55

FBI yachunguza usalama wa Wanajeshi 25,000 wanaoimarisha ulinzi Washington


Baadhi ya Walinzi wa Kitaifa wakiimarisha usalama mjini Washington, DC on January 17, 2021 baada ya makundi yenye msimamo mkali yanayo muunga mkono Rais Donald Trump kuitisha maandamano nchi nzima hapa Marekani.
Baadhi ya Walinzi wa Kitaifa wakiimarisha usalama mjini Washington, DC on January 17, 2021 baada ya makundi yenye msimamo mkali yanayo muunga mkono Rais Donald Trump kuitisha maandamano nchi nzima hapa Marekani.

Wakati Rais mteule wa Marekani Joe Biden akijiandaa kuapishwa Jumatano, idara ya serikali kuu ya upelelezi - FBI inafanya uchunguzi wa usalama wa Wanajeshi 25,000.

Wanajeshi hao wamepelekwa kuulinda mji wa Washington katika hafla ya kuapishwa Biden wakati ukiwepo wasiwasi wa kuwepo shambulio la ndani lililohamasishwa na wafuasi wa Rais Donald Trump.

Waziri wa Ulinzi Ryan McCarthy aliwaambia shirika la habari la AP kuwa yeye na viongozi wengine hawajaona ushahidi wowote wa vitisho vyovyote.

Ameongeza kuwa hadi sasa uchunguzi wao haukuonyesha dalaili ya kuwepo matatizo yoyote kati ya wanajeshi hao.

“Tunaendelea kupitia mchakato huo, na kuchukua mtazamo wa pili, na wa tatu kwa kila mmoja aliopewa nafasi ya kushiriki katika operesheni hii," McCarthy alisema.

McCarthy alisema kuna ripoti za kiintelijensia zinazoonyesha kuwa kuna vikundi vya nje vinavyo andaa maandamano ya silaha kabla ya siku ya kuapishwa.

XS
SM
MD
LG