Ripoti hiyo inasema pande hizo mbili zilishiriki uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini, karibu mwaka mmoja uliopita.
Tume hiyo yenye wajumbe watatu iliwasilisha ripoti ya kurasa 21 kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya katika maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia ambayo yameshuhudia maovu mengi yaliyofanywa tangu mzozo kati ya serikali na chama cha Ukombozi cha Tigray, kuzuka Novemba 3, 2020. Akiwasilisha ripoti hiyo, mwenyekiti wa tume hiyo, Mohamed Chande Othman, alionya kwamba kushindwa kwa makubaliano ya mwaka jana ya kumaliza uhasama, kumevunja matumaini kwamba mkataba huo "utafungua njia ya kumaliza moja ya migogoro mibaya zaidi ya karne ya 21, ambayo imevuruga jamii kote kaskazini mwa Ethiopia
." Umoja wa Mataifa na taasisi zingine zinakadiria takriban watu 600,000 katika jimbo la Tigray walikufa na zaidi ya milioni 2 walilazimika kuyahama makazi yao kati ya Novemba 2020 na Agosti 2022.
Forum