Vyombo vya habari Misri vinaripoti kuwepo na idadi kubwa ya majeruhi mjini Cairo baada ya vikosi vya usalama kushambulia maeneo mawili walokusanyika wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi.
Vikosi vya usalama Misri vya pambana na wafuasi wa Morsi

1
Afisa wa usalama abishana na mama mmoja anabeba fimbo katika eneo ambalo wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi wamekusanyika katibu na Chuo kikuu cha Cairo, huko Giza, Cairo,, Augusti 14, 2014.

2
Wafuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wakizingira gari la polisi wakati wa mapambano na vikosi vya usalama vya Misri katika mtaa wa Cairo wa Mohandessin, Misri, Augusti 14, 2013.

3
Wafuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wakiimba nyimbo dhidi ya waziri wa ulinzi Gen. Abdel-Fattah el-Sissi wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika mtaa wa Cairo wa Mohandessin , Augusti 14, 2013.

4
Gari la polisi linasukumwa na kunagushwa kutoka daraja la October 6 na waandamanaji karibu na kambi kuu la mkusanyiko mkubwa wa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi katika wilaya ya Nasr City mashariki ya Cairo, Augusti 14, 2013.