Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:28

Ebrahim Raisi ashinda uchaguzi wa rais Iran


Rais mteule Ebrahim Raisi
Rais mteule Ebrahim Raisi

Mgombea kiti cha rais mwenye msimamo wa wastani nchini Iran Abdolnasser Hemmati, amekiri kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika jana Ijumaa na Imam mwezye itikadi kali za kihafidhina, mwanasheria mkuu Ebrahim Raisi.

Maafisa wa uchaguzi wa Iran wanasema, Raisi alipata asilimia 62 za kura baada ya asilimia 90 za kura kuhesabiwa, na kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo.

Shirika la habari la Fars News liliripoti mapema kwamba ni asilimia 37 tu ya wapigaji kura milioni 59 wa taifa hilo walioshiriki kwenye uchaguzi ambao ulishuhudia wagombea kadhaa wakijitoa kabla ya siku ya kupiga kura.

Wachambuzi wanasema uchaguzi huu haujawavutia wa Iran ambao wengi wamekasirishwa na ulaji rushwa, na usimamizi mbaya wa uchumi uliobanwa kutokana na vikwazo vya kiuchumi vya Marekani.

Rais anayemaliza muda wake Hassan Rouhani
Rais anayemaliza muda wake Hassan Rouhani


Rais ​Hassan Rouhani mwenye msimamo wa wastani anaeondoka madarakani baada ya mihula miwili, amewapongeza wananchi kwa kumchagua mtu waliompenda atakaye chukua madaraka mwezi Agosti.

Viongozi mbalimbali wa nchi za Kiarabu na dunia wanapeleka ujumbe wa pongezi kutokana na ushindi wa Raisi.

XS
SM
MD
LG