Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 13:52

DRC yaripoti maambukizi mapya 92 kwa siku moja Jumatano


Rais Felix Tshisekedi alipokutana na viongozi wa dini, Kinshasa, Aprili 20, 2020. (Facebook/présidence RDC)

Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha watu wengine 92 wameambukizwa virusi vya corona kulingana na vipimo vilivyofanywa siku moja na idadi Jumatano imefikia 797.

Idadi hiyo ndio ya juu zaidi nchini humo kutangazwa kwa siku moja, tangu nchi hiyo ilipotangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya corona, mwezi Machi.

Watu 69 wamethibitishwa kuambukizwa katika mji mkuu wa Kinshasa na 23 katika mkoa wa kati ya Congo.

Watu wengine 212 wanachunguzwa kubaini iwapo wameambukizwa virusi hivyo.

Watu 104 wakiwemo wafungwa na walinzi wa magereza, wameambukizwa corona katika gereza la Ndolo, mjini Kinshasa.

Waziri wa Afya ya Umma Eteni Longondo, amesema hali imedhibitiwa, licha ya ongezeko la idadi ya watu wanaoambukizwa. Amesema kwamba serikali inafikiria kufungua shule.

Kufikia sasa, watu 705 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na 34 kuaga dunia, nchini DRC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG