Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:56

DRC : Mtu mwengine aliyemtuhumu mke wa rais kwa kupora msaada akamatwa

Mke wa Rais wa DRC Denise Nyakeru Tshisekedi akihudhuria ibada maalum Kinshasa, Mei 31, 2021, kuwaombea wale walioathirika na mlipuko wa volcano uliotokea Mei 22, 2021.(Photo by Arsene Mpiana / AFP)
Mke wa Rais wa DRC Denise Nyakeru Tshisekedi akihudhuria ibada maalum Kinshasa, Mei 31, 2021, kuwaombea wale walioathirika na mlipuko wa volcano uliotokea Mei 22, 2021.(Photo by Arsene Mpiana / AFP)

Mwanachama wa pili wa kundi la kupambana na ulaji rushwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Ghislain Muhiwa amekamatwa baada ya kumtuhumu mke wa Rais Felix Tshisekedi kwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Kundi la vijana la kupigania mageuzi, maarufu kama Lucha, linatuhumu kwamba taasisi inayoisimamiwa na mke wa Rais, Denise Tshisekedi, imepora msaada uliyokuwa umelengwa kuwapa waathiriwa wa mlipuko wa volcano katika mlima Nyiragongo, mashariki wa nchi DRC.

Taasisi ya mke wa Rais imekanusha tuhuma hizo.

Mtuhumiwa alikamtwa akiwa anaelekea kupeleka mahari kwa wakwe zake mjini Goma.

Mwenzake Parfait Muhani alikamatwa mwezi Julai kwa madai hayo hayo anasubiri kesi yake mbele ya mahakama ya kijeshi.

XS
SM
MD
LG