Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:57

Mwandishi wa habari auawa DRC


Ramani inayoonyeha wilaya ya Rutshuru, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ramani inayoonyeha wilaya ya Rutshuru, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la taifa nchini DRC, ameuawa kwa kukatwa shingo katika jimbo la Kivu Kaskazini, lililo Mashariki mwa nchi hiyo, ambako mauaji na mapigano yanayohusishwa na vikundi vyenye silaha, yamekuwa yakiendelesa kwa miaka kadhaa.

Heritier Magayane, mwenye umri wa miaka 26, ambaye alikuwa ameoa na alikuwa baba wa watoto wawili, alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Redio na Television cha kitaifa, katika wilaya ya Rutshuru tangu mwaka wa 2018, mwenzake Roger Sebyeradu aliliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Magayane alipokea simu kutoka kwa mtu ambaye alipanga mahali pa kukutana naye na hapo ndipo alipouawa usiku wa Jumamosi, koo lake lilikatwa, alisema Luc Albert Bakole Nyengeke, afisa wa jeshi anayesimamia utawala katika wilaya ya Rutshuru.

XS
SM
MD
LG