Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:36

Marekani yaisaidia DRC dola milioni moja kwenye sekta ya madini


Mfano wa eneo la uchimbaji madini
Mfano wa eneo la uchimbaji madini

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa baada ya mkutano kati ya balozi wa Marekani, Hammer na naibu waziri wa madini, Godard Motemona inaeleza kwamba msaada huo utatumiwa kuimarisha miradi iliyopo hasa ule wa kupambana na kuwafanyisha kazi watoto kwenye migodi ya madini ya Cobalt

Marekani imetangaza kwamba inaongeza msaada wa karibu dola milioni moja kwa ajili ya miradi ya kuimarisha uchimbaji madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa baada ya mkutano kati ya balozi wa Marekani, Hammer na naibu waziri wa madini, Godard Motemona inaeleza kwamba msaada huo utatumiwa kuimarisha miradi iliyopo hasa ule wa kupambana na kuwafanyisha kazi watoto kwenye migodi ya madini ya Cobalt.

Msaada huo mpya unaotolewa na wizara ya kazi ya Marekani unafikisha msaada wa jumla ya dola milioni 3.5 kugharimia miradi yote. Balozi Hammer amesisitiza juu ya haja ya utawala bora na misada iliyopo inayosimamiwa na idara ya Marekani ya maendeleo ya kimataifa ili kuimarisha ufundi wa kuchimba madini kwa lengo la kupunguza migogoro.

XS
SM
MD
LG