Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:08

UNESCO yasifu DRC kwa kutunza mbuga ya Salongo


Picha ya ndovu wakiwa mbugani
Picha ya ndovu wakiwa mbugani

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Jumatatu imeonekana kupata ushindi mkubwa wa kimazingira baada ya baraza la Umoja wa mataifa la UNESCO kuondoa moja wapo ya mbuga zake kwenye orodha ya zile zilizo hatarini.

UNESCO imelisifu taifa hilo kwa juhudi zake za kulinda bustani ya Salonga, kwa kuzuia uchimbaji mafuta. Taarifa kutoka UNESCO inasema kuwa kulindwa kwa mbuga hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi ya umma nchini humo, kumesababisha ongezeko la idadi ya nyani wanaojulikana kama bonobo pamoja na ndovu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wizara ya mazingira ya DRC imekaribisha hatua hiyo ikisema kupitia taarifa kwamba sasa ni wakati wa kufikiria kwa kina kuhusu kulinda mazingira. Mbuga ya Salongo ndiyo kubwa zaidi barani Afrika ikiwa nyumbani kwa asilimia 40 ya nyani aina ya bonobo walioko ulimwenguni.

Mbuga hiyo ilibuniwa 1970 na kiongozi dikteta Mobutu Sese Seko lakini ikawekwa kwenye orodha ya zile zilizo hatarini mwaka wa 1984. Kando na nyani wa bonobo, kuna wanyama wengine wengi pamoja na ndege wa kuvutia kama tausi wa Congo.

XS
SM
MD
LG