Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:55

COVID-19 : Papa Francis atoa wito ulimwengu kushikamana kufufua uchumi


Papa Francis akibadilishana zawadi na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban, katika Jumba la Makumbusho la Sanaa Budapest, Jumapili, Septemba 12, 2021.
Papa Francis akibadilishana zawadi na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban, katika Jumba la Makumbusho la Sanaa Budapest, Jumapili, Septemba 12, 2021.

Papa Francis ameitaka Ulaya kuonyesha mshikamano kote ulimwenguni wakati wa kufufua uchumi kutokana na janga la Covid-19, aliongea hayo akiwa katika ziara nchini Slovakia moja ya nchi zilizoathirika zaidi barani Ulaya.

Katika safari yake ya kwanza ya nje tangu operesheni ya utumbo mpana mwezi Julai, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 84 aliliita janga hilo "mtihani mkubwa wa wakati wetu ".

“Imetufundisha jinsi ilivyo rahisi, hata wakati sisi sote tuko kwenye mashua moja, kujiondoa na kujifikiria wenyewe," alisema.

Slovakia, mwanachama wa Umoja wa Ulaya ina idadi ya watu milioni 5.4, ilikuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya Covid-19 na vifo ulimwenguni kwa wiki kadhaa mwaka huu.

Baada ya miezi mingi na yenye majaribu ya janga , tukijua kabisa shida tutakazokabiliwa nazo tunatarajia kwa matumaini mabadiliko ya kiuchumi yanayopewa nafasinzuri na mipango ya kufufua na Jumoja wa Ulaya, "Papa alisema katika mji mkuu wa Slovakia, Bratislava.

XS
SM
MD
LG