Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 21:28

Papa Francis ametolewa hospitali huko Roma


Papa Francis aliongoza sala akiwa kwenye kibaraza cha hospitali ya Gemelli huko Roma
Papa Francis aliongoza sala akiwa kwenye kibaraza cha hospitali ya Gemelli huko Roma

Papa Francis aliondolewa nusu ya utumbo wake hapo Julai nne ukiwa ni upasuaji wake mkubwa wa kwanza tangu ashike madaraka ya kuwa Papa mwaka 2013

Papa Francis ameonekana akiondoka hospitali siku ya 10 baada ya kufanyiwa upasuaji ambao uliondoa nusu ya utumbo wake.

Walioshuhudia walisema gari lililokuwa limembeba Papa Francis lilionekana likiondoka katika hospitali ya Gemelli Polytechnic mjini Roma, Jumatano asubuhi.

Papa Francis aliondolewa nusu ya utumbo wake hapo Julai nne upasuaji wake mkubwa wa kwanza tangu ashike madaraka ya kuwa Papa mwaka 2013. Ulikuwa utaratibu uliopangwa mapema hapo Julai, wakati maombi ya Papa Francis yalipositishwa kwa muda kwa kawaida Papa anachukua muda wa mapumziko.

XS
SM
MD
LG