Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:12

Upasuaji : Vatican yasema Papa Francis anaendelea vizuri


FILE PHOTO: Papa Francis baada ya kukutana na waumini.

Maafisa wa Kanisa Katoliki mjini Vatican wamesema Jumatatu Papa Francis yuko katika hali nzuri bila ya kuhitaji msaada wa kupumua na anaendelea vyema baada ya upasuaji wa kutoa nusu ya utumbo. 

Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema Papa Francis mwenye umri wa miaka 84 anatarajiwa kubaki hospital ya Gemelii Polyclinic, mjini Rome, kwa siku saba akipatiwa matibabu.

Taarifa fupi ya afya iliyotolewa na Vatican Jumatatu baada ya saa 12 za upasuaji hapo Jumapili imeeleza hayo.

Habari za kulazwa kwa Papa Francis ziliwashangaza watu wengu duniani na maafisa wa Kanisa Katoliki wanasema hilo ni kwa sababu yeye mwenyewe alitaka hali yake ya afya iwe ni jambo la faragha.

Upasuaji wanasema ulihitajika na ilikuwa ni kutoa sehemu ya utumbo mdogo na kuunganisha tena na utumbo makubwa.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG