Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:24

COVID-19: Ottawa yatangaza hali ya dharura


FILE - Maafisa wa polisi wakiwa na waandamanaji mbele ya jengo la Bunge wakati wenye magari na wafuasi wao wanaopinga masharti ya COVID-19 na kuchanja, Ottawa, Canada, Feb. 6, 2022.
FILE - Maafisa wa polisi wakiwa na waandamanaji mbele ya jengo la Bunge wakati wenye magari na wafuasi wao wanaopinga masharti ya COVID-19 na kuchanja, Ottawa, Canada, Feb. 6, 2022.

Meya wa mji mkuu wa Canada ametangaza hali ya dharura Jumapili wakati waandamanaji wanaopinga masharti ya COVID 19 wanaendelea kuudumaza mji wa Ottawa.

Meya Jim Waston amesema tangazo hilo linazingatia uungwaji mkono kutoka kwenye mamlaka nyingine na nyanja za serikali.

Inatoa mamlaka ya ziada katika mji na manunuzi na jinsi inavyotoa huduma ambayo huenda itasaidia kununua vifaa vinavyohitajika na wafanyakazi walioko mstari wa mbele na wanaojibu kwanza wakati wa janga.

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika tena Ottawa kwa mara nyingine tena mwishoni mwa wiki wakiungana na mamia wengine waliokuwa kimya tangu mwisho wa wiki iliyopita.

Wakazi wa Ottawa wamegadhabishwa na kutokoma kwa honi za magari, usumbufu, manyanyaso na hofu kuwa hakuna mwisho unaoonekana baada ya mkuu wa polisi kusema kuwa ni “ kuzingirwa “ ambako hakuweza kudhibiti.

XS
SM
MD
LG