Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:17

COP27: Guterres aonya kuhusu "ahela ya hali ya hewa"


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonia Guterres akihutubia kongamano la COP27 nchini Misri.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonia Guterres akihutubia kongamano la COP27 nchini Misri.

Mkutano mkuu wa hali ya hewa duniani unaendelea katika mji wa Sharm el-Shekih, nchini Misri, ambako Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya  kwamba mataifa ya dunia, haswa yale tajiri zaidi, lazima yachukue hatua za haraka kuepusha uharibifu wa ikolojia.

"Tuko kwenye barabara kuu ya kwenda ahela ya hali ya hewa na tunaendelea kuongeza kasi kwelekea huko," Guterres alisema katika hotuba yaka kwenye mazungumzo hayo ya kimataifa, ambayo hufanyika kila mwaka ya kimataifa yankiongozwa na Umoja wa Mataifa.

"Tuko kwenye mapambano ya maisha yetu, na tunashindwa katika vita hivi," aliongeza Guterres.

Suala muhimu katika majadiliano mwaka huu ni jinsi na kwa kiwango gani nchi tajiri zaidi duniani, zilizoendelea kiviwanda ambazo zinachangia sehemu kubwa zaidi ya utoaji wa gesi chafuzi, ikiwa ni pamoja na Marekani, zinahitajika kusaidia mataifa maskini ambayo mara nyingi hubeba mzigo mkubwa wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi Jumapili huku Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani likisema kwamba kuna uwezekano Dunia imeshuhudia miaka minane ya joto zaidi katika rekodi, ambayo ni pamoja na kipindi ambacho mataifa ya dunia yalipitisha makubaliano ya kihistoria ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Paris mwaka 2015.

Makubaliano hayo yametaka kupunguzwa kwa kasi kwa uzalishaji wa gesi chafu na mageuzi kuelekea vyanzo vya nishati safi na kupunguza matumizi ya nishati ya yenye madhara makubwa, ili kupunguza kasi ya ongezeko la joto duniani.

Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi wa nchi na serikali mbalimbali, na wadau wengine kutoka kote duniani.

XS
SM
MD
LG