Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:53

Waziri Blinken aishukuru Misri kwa uongozi wa masuala ya hali ya hewa


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokuwa katika mkutano mjini Jerusalem, Machi 27, 2022. (AP).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokuwa katika mkutano mjini Jerusalem, Machi 27, 2022. (AP).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezungumza Alhamisi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Hali ya hewa  (COP27) wa 2022 mwezi huu huko Sharm El-Sheikh.

Waziri huyo alieleza shukrani zake za dhati kwa uongozi wa masuala ya hali ya hewa wa Misri na kujitolea kwa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati wa Marekani na Misri, ambao unaimarishwa na maendeleo yanayoonekana juu ya haki za binadamu nchini Misri.

Kuhusiana na hili, alipongeza taarifa ya kuachiliwa katika miezi iliyotangulia kwa idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa, na alitoa sauti ya kuunga mkono msamaha huo na kuachiliwa, pamoja na hatua za kuimarisha mchakato unaofaa wa sheria na ulinzi kwa uhuru wa kimsingi kwa wote.

Waziri huyo alisisitiza tena michango muhimu ya mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na kwa mafanikio ya COP27.

Waziri Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje Shoukry pia walijadili juhudi za pamoja za kuendeleza amani ya kikanda, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono uchaguzi nchini Libya, na juhudi zinazoendelea za kuhakikisha hatua sawa za ustawi, usalama, na heshima kwa Waisraeli na Wapalestina.

XS
SM
MD
LG