Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:44

Chile yapata rais kijana aliyeshinda kwa kura asilimia 56


Rais mteule wa Chile Gabric Boric
Rais mteule wa Chile Gabric Boric

Mbunge wa mrengo wa kushoto aliyepata umaarufu wakati wa maandamano ya kuipinga serikali huko Chile amechaguliwa rais ajaye wa nchi hiyo.

Huku karibu asilimia 99 ya vituo vya kupigia kura vikiripoti, Gabric Boric ameshinda kwa asilimia 56 ya kura ikilinganishwa na asilimia 44 dhidi ya mpinzani wake mkonsevativu Jose Antonio Kast.

Gabriel Boric, rais ajaye anaeleza : "Mabadiliko ya hali ya hewa, wapendwa wenzangu siyo uvumbuzi. Yako hapa, na yameonyesha matokeo ya moja kwa moja katika maisha yetu na ya kizazi kijacho.

Siyo bahati mbaya kwamba ni vijana wadogo duniani ndyo waliopaza sauti zao, kuanzia kwa Greata hadi kwa Julieta hapa Chile, Julieta, mbele ya nguvu zinazoendelea kuwaangamiza, kuiharibu dunia ni kujiharibu wenyewe, hatutaki tena maeneo ya kujitoa muhanga, hatutaki tena miradi ambayo inaiharibu Chile yetu, amabyo inaharibu jumuiya yetu na kuitolea mfano.”

Akiwa na umri wa miaka 35 Boric atakuwa rais kijana kuliko marais wote wa chile waliotangulia.

Rais anayeondoka madarakani Sebastian Pinera mkonsevativu bilionea alifanya mkutano kwa njia ya video na Boric kuahidi ushirikiano wa serikali yake katika kipindi cha miezi mitatu ya mpito.

XS
SM
MD
LG