Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 09:51

Chile kufanya uchaguzi kati ya wagombea wenye siasa kali za mrengo wa kulia na kushoto

Wagombea urais wa Chile Gabriel Boric, wa muungano wa mrengo wa kushoto 'Apruebo Dignidad, na Jose Antonio Kast wa chama cha Republican cha mrengo mkali wa kulia, wakipiga picha kabla ya mdahalo wa moja kwa moja wa televisheni kuelekea uchaguzi wa rais.REUTERS

Chile inafanya uchaguzi Jumapili kati ya wagombea wa siasa kali za mrengo wa kulia na wa mrengo wa kushoto kutafuta rais wa kuongoza nchi hiyo kupitia kipindi cha mabadiliko ya katiba huku kukiwa na kelele za kutaka mageuzi ya kijamii.

Nchi hiyo yenye watu milioni 19 iko ukingoni, ikihofia maandamano ya umma kuibuka tena kujibu matokeo ya mbio zenye ushindani mkali kati ya wakili wa kiconservative Jose Antonio Kast, mwenye umri wa miaka 55 na mwanaharakati wa zamani wa wanafunzi Gabriel Boric, kijana aliye miaka 20 chini yake.

Kwa nchi ambayo imepiga kura kwa mrengo wa kati tangu kuondolewa madarakani kidemokrasia kwa dikteta katili Augusto Pinochet miaka 31 iliyopita, kuna tofauti kubwa kati ya watu wawili walio nje ya siasa mmoja akiahidi hali ya ustawi wa kijamii, na mwingine muendelezo wa mtindo wa uchumi wa kiliberali wa Chile.

Wengi wanaogopa sera za kiconservative za kijamii na kifedha za mgombea Kast anayemuunga mkono Pinochet, kupinga ndoa za mashoga na utoaji mimba, na mtetezi wa kupunguza kodi na matumizi ya kijamii.

XS
SM
MD
LG