Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:10

Marekani yajiondoka kwa mkataba wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa


Marekani imejiondoa rasmi kutoka kwa mkataba wa Paris wa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatua hiyo inatimiza ahadi ya rais Donald Trump ya kuiondoa Marekani ambayo ndio mchafuzi mkubwa wa hewa kote duniani, kutoka kwa mkataba huo.

Hata hivyo, aliyekuwa makam wa rais Joe Biden, ameahidi kurejesha Marekani kwenye mkataba huo, endapo atashinda uchaguzi mkuu, ambao matokeo yake bado yanasubiriwa.

Rais Donald Trump alitangaza nia ya kuindoa Marekani kutoka mkataba huo, June 2017, kwa madai kwamba unaathiri uchumi wa Marekani.

Marekani inakuwa nchi pekee kati ya wanachama 197 kujitoa kwenye mkataba huo wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ulioundwa mwaka 2015.

Uingereza, Ufaransa, Chile na Italy, zimesema kwamba hatua ya Marekani ni ya kusikitisha.

XS
SM
MD
LG