Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:05

Chanjo ya COVID-19: Aspen Pharmacare yafikia makubaliano na Johnson & Johnson


FILE PHOTO: Nembo ya Aspen Pharmacare (Picha na Reuters)
FILE PHOTO: Nembo ya Aspen Pharmacare (Picha na Reuters)

Kampuni kubwa ya kutengeneza dawa ya Afrika Kusini Aspen Pharmacare Jumanne imekamilisha makubaliano na kampuni ya Johnson & Johnson kwa ajili ya kufunga, kuuza na kusambaza chanjo ya COVID 19 ya marekani chini ya chapa yake barani Afrika.

Mwezi Novemba Aspen iliingia kwenye mazungumzo na J&J kwa mpango wa leseni ambao utatoa uhuru wa kuuza na kusambaza chanjo chini ya chapa yake yenyewe.

Mkataba huo pia unairuhusu Aspen kujadili kupanua makubaliano ya kujumuisha matokeo yoyote mapya ya dawa kama zile zinazo tengenezwa kwa ajili ya maambukizo mapya ili kutolewa kama Booster, Aspen imesema katika taarifa yake.

J&J imeingia mkataba wa kufunga dawa za chanjo ya COVID 19 katika dozi za mwisho utaratibu unaoitwa kujaza na kumaliza, na kusambaza kwa J&J.

Hata hivyo haijaipa Aspen haki ya nani anayetakiwa kupata chanjo na wapi zinakwenda.

Katika taarifa tofauti J&J imesema mkataba unamaanisha kwamba Aspen hivi sasa inaweza kusambaza chanjo ya COVID 19 chini ya mpango wa Aspenovax katika nchi zote 55 za Afrika na vyombo vyote vya kimataifa vinavyounga mkono mpango wa chanjo ya Afrika.

XS
SM
MD
LG