Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:24

 Takriban dozi laki moja za chanjo ya Pfizer ziko hatarini kuharibiwa-Mamlaka Afrika kusini


Chanjo ya Pfizer/BioNTech ya COVID-19.
Chanjo ya Pfizer/BioNTech ya COVID-19.

Mamlaka ya afya ya Afrika Kusini ilisema  Ijumaa kamba  takriban dozi 100,000 za chanjo ya Pfizer ya COVID-19 ziko katika hatari ya kuharibiwa ifikapo mwishoni  mwa mwezi huu kutokana na watu kutojitokeza kwa haraka kupokea chanjo.

Afrika Kusini imerekodi idadi kubwa ya maambukizi na vifo vya corona katika bara la Afrika, hata hivyo utoaji chanjo umepungua na nchi ina akiba ya kutosha ya chanjo ya dozi milioni 25.

Waziri wa Afya Joe Phaahla aliambia mkutano wa wanahabari mtandaoni kamba kuna hatari karibu dozi 100,000 au zaidi ambazo zitaisha muda wake mwishoni mwa Machi na zitatupwa. Akiongezea kusema kua Itakuwa siku ya kusikitisha ikiwa kiasi kikubwa cha dozi kinaweza kutupwa.

XS
SM
MD
LG