Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:51

Afrika Kusini yabadilisha kanuni za kupokea chanjo ya COVID-19


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imesema Jumatatu kwamba inabadilisha kanuni za chanjo ya COVID-19 kwa ajili ya kusaidia kuongeza kasi ya uchomaji wa chanjo hiyo wakati maambukizi yamepungua na nchi ina chanjo za kutosha.

Serikali imepunguza muda wa kuchoma dozi ya kwanza na ya pili ya chanjo ya PFIZER kutoka siku 42 hadi 21 na itaruhusu watu ambao wamepokea dozi mbili za chanjo ya Pfizer kuchoma booster miezi mitatu baada ya dozi ya pili tofauti na ilivyokuwa kusubiri kwa miezi sita.

Pia itatoa chaguo kuchanganya na kuoanisha booster kwa watu wazima ambao walipata chanjo moja ya J&J au Pfizer miezi miwili baada ya dozi zao.

Watu wazima waliopata chanjo ya Pfizer wataruhusiwa kupokea chanjo ya J&J pamoja na Pfizer kama dozi ya tatu.

Afrika Kusini imerekodi kesi nyingi za maambukizi na vifo katika bara la Afrika.

Hadi sasa tayari imetoa chanjo kwa asilimia 28 ya watu wake takriban milioni 60.

Asilimia hiyo ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi yoyote ya bara la Afrikia ingawa haijafikia malengo ya serikali.

XS
SM
MD
LG