Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:11

Chama cha Wauguzi chaikosoa CDC kwa tamko la kutokuvaa barakoa


Makao makuu ya CDC, Atlanta, Marekani.

Chama kikuu cha wauguzi nchini Marekani kimeshutumu tangazo la karibuni la Vituo vya kudhibiti magonjwa kwamba watu waliopatiwa dozi kamili ya chanjo za Covid hawana haja ya kuvaa barakoa katika sehemu mbali mbali.

Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Kitaifa wa Wauguzi, Bonnie Castillo amesema huu muongozo mpya wa CDC haulingani na sayansi, na haulindi afya ya umma na kutishia maisha ya wagonjwa.

Pia amesema muongozo huu haulindi maisha ya wauguzi na wafanyakazi wengine wa mstari wa mbele kote nchini na kuongezea huu si wakati wa kulegeza masharti ya kujilinda.

Mkurugenzi huyo alionyesha hasira juu ya hatua hiyo ya CDC, akihoji vipi wanafanya maamuzi kama hayo wakati bado Marekani ipo katikati ya janga baya sana kuwahi kutokea.

Rais wa umoja huo Jean Ross amesema kama CDC imetambua vyema sayansi ya jinsi virusi hivi vinavyoambukiza, huu muongozo mpya kamwe usingetolewa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG