Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:30

Burundi yasema imewaua 'wahalifu' 22 waliokuwa wanataka kuleta machafuko


Rais Pierre Nkurunziza

Serikali ya Burundi imesema Jumanne imewaua “wahalifu” wasiopungua 22 katika eneo la milimani linalokabili mji mkuu wa Bujumbura tangu wiki iliyopita, katika kile ilichoeleza kuwa ni uhalifu unafungamana na uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Mei 2020.

Vyombo vya usalama vimesema askari wawili wa jeshi la polisi waliuawa na watu sita waliowashambulia kukamatwa.

Mapambano hayo yalitokea baada ya wakazi wa eneo kuwatahadharisha polisi kuwepo kwa darzeni ya watu wenye silaha waliojificha katika mashamba ya kahawa wilaya ya Nyabiraba, kiongozi wa eneo ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwa sharti la kutotajwa jina lake.

Polisi wamesema mapigano pia yalienea katika wilaya ya jirani ya Isare.

“Wahalifu walikuwa wanatumia fursa ya kipindi hiki cha uchaguzi wakidhani watu watakuwa hawako makini,” msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye alisema kupitia shirika la utangazaji la serikali RTNB.

“Wananchi wametakiwa kuwa na utulivu kwa sababu maafisa wa usalama wanaendelea kuimarisha ulinzi.”

Burundi, ambayo inajumuisha makabila kama yale ya nchi jirani ya Rwanda, imepitia misukosuko ya kiukabila na vurugu za kisiasa kwa miongo kadhaa, ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1993-2005 ambapo watu 300,000 wengi wao raia waliuawa.

Uchaguzi wa mwezi Mei utamchagua mrithi wa Rais Pierre Nkurunziza, kiongozi wa zamani wa waasi ambaye amekuwa madarakani tangu 2005.

Awamu tatu za utawala wake umeshuhudia uvunjifu wa Amani mara kwa mara na tuhuma za kimataifa juu ya uvunjifu wa haki za binadamu, jambo ambalo serikali yake inakanusha.

Katika uchaguzi huu, mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, jenerali wa jeshi mstaafu ambaye anaongoza kitengo cha masuala ya kijeshi katika ofisi ya rais, atachuana na kiongozi wa zamani wa waasi, Agathon Rwasa, wa chama cha upinzani cha CNL.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG