Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:29

Afrika Mashariki yalaani jaribio la mapinduzi Burundi


Watu wakifurahia mjini Bujumbura ripoti kuwa Rais Nkurunziza amepinduliwa mapema Jumatano.
Watu wakifurahia mjini Bujumbura ripoti kuwa Rais Nkurunziza amepinduliwa mapema Jumatano.

Viongozi wa Afrika mashariki wamelaani kile walichoita jaribio la mapinduzi Burundi Jumatano na Jenerali mmoja ambaye ametangaza kumwondoa madarakani Rais Pierre Nkurunziza kwa kujaribu kugombani urais kwa awamu ya tatu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jakaya Kikwete wa Tanzania
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jakaya Kikwete wa Tanzania

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki Rais Jakaya Kikwete of Tanzania alisema katika taarifa baada ya mkutano kuwa viongozi hao wa mataifa matano ya Afrika Mashariki inyojumuisha nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania na Burundi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania alisema Nkurunziza hakuingia ndani ya mkutano huo na aliondoka Tanzania kurejea Burundi.

Meja-Jenerali Godefroid Niyombare ambaye alitangaza kumwondoa madarakani Nkurunziza alisema mjini Bujumbura kuwa uwanja wa ndege wa Bujumbura na maeneo mengine ya kuvuka mpaka yamefungwa.

XS
SM
MD
LG