Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 21:41

Jenerali asema amemwondoa madarakani Rais Nkurunziza Burundi


Polisi wakijaribu kuzuia maandamano Bujumbura

Jenerali mmoja wa Burundi anasema amemwondoa madarakani Rais Pierre Nkurunzinza ambaye yuko nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika mashariki kuhusu hali ya Burundi.

Jenerali Godefroid Niyombare alitoa matangazo katika radio kadha za kibinafsi nchini humo Jumatano.

Mwandishi wa Sauti ya America aliyeko mjini Bujumbura anasema hakuna uhakika kama Jenerali huyo anaungwa mkono kikamilifu na jeshi. Kumekuwa na ripoti za milio ya bunduki siku nzima mjini Bujumbura wakati polisi wanapambana na waandamanaji.

Jaribio hilo la mapinduzi limetokea baada ya wiki kadha za mvutano tangu rais atangaze kuwa atagombania urais kwa awamu ya tatu.

Rais Nkurunzinza aliondoka Bujumbura Jumatano kwenda Dar es Salaam, Tanzania, ambako viongozi wa nchi za Afrika mashariki wanakutana kujadili hali ya kisiasa Burundi.

XS
SM
MD
LG