Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:48

Mwingine auawa katika ghasia Burundi


Bus likiwaka moto baada ya kuchomwa na waandamanaji Ngagara, nje kidogo ya Bujumbura
Bus likiwaka moto baada ya kuchomwa na waandamanaji Ngagara, nje kidogo ya Bujumbura

Mtu mwingine aliuawa Jumanne Burundi na kufanya idadi ya watu waliokufa kufikia 15 katika ghasia zinazoendelea Bujumbura kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kugombania tena urais nchini humo.

Polisi mmoja mwanamke alikuwa miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ghasia za Jumanne. Zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa katika ghasia hizo mpaka sasa, ikiwa ni wiki ya tatu ya machafuko.

Machafuko haya yanaendelea huku viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitazamiwa kuanza mkutano wa dharura Jumatano mjini Dar es Salaam kujadili ghasia za Burundi.

Waziri mdogo wa maswala ya Afrika wa Marekani Linda Thomas-Greenfield.
Waziri mdogo wa maswala ya Afrika wa Marekani Linda Thomas-Greenfield.

Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia maswala ya Afrika, Linda Thomas-Greenfiled, pia atahudhuria mkutano huo kuunga mkono juhudi za viongozi wa Afrika mashariki, taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema.

Thomas-Greenfield anatazamiwa kueleza wasiwasi wa Marekani kuhusu hali ya Burundi pamoja na kuunga mkono Mkataba wa Arusha na mazungumzo ya pande zote kuhakikisha amani na uchaguzi unaojumuisha watu wote Burundi.

Wengi wanasema uamuzi wa Nkurunzinza kuwania tena urais ni kuvunja mkataba wa Arusha ambao ulimaliza vita nchini Burundi.

Zaidi ya watu 50,000 wamekimbia Burundi kuelekea nchi jirani za Tanzania na Rwanda kwa hofu kuwa zinaweza kuzuka ghasia kubwa katika uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG