Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:19

Burkina Faso yakata tiketi ya kuingia Nusu fainali


Mashabiki wa soka wa Burkina Faso mjini Ouagadougou wakishangilia ushindi wa timu yao.
Mashabiki wa soka wa Burkina Faso mjini Ouagadougou wakishangilia ushindi wa timu yao.

Burkina Faso imekata tiketi  ya kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya afrika AFCON baada ya kuibwaga Tunisia Simba wa Atlas kwa bao 1-0 katika uwanja wa Garoua Jumamosi.

Alikuwa ni mchezaji mdogo kuliko wote katika michuano hiyo Dango Outtara kinda wa miaka 19 aliyekuwa shujaa wa Burkina Faso anayecheza katika timu ya Lorient ya Ufaransa aliyepachika bao katika dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza.

Burkina Faso walipata pigo katika dakika ya 82 wakati mfungaji huyo Dango Outtara alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumgonga beki wa Tunisia na kiwiko wakati akiruka kupiga kichwa .

Kabla ya kutoa nyekundu refa alimpa kadi ya njano lakini baada ya kuangalia kwa kina akitumia VAR alibadili msimamo na kufuta kadi ile ya njano na kutoa nyekundu.

Kulitokea tukio lisilo la kawaida kwa refa huyo kutoa kadi kwa mchezaji asiyecheza uwanjani kunako dakika ya 85 wakati mchezaji wa akiba wa Burkina Faso Hassane Bande alipigwa kadi ya njano kwa kosa la kuficha mpira uliotoka nje akituhumiwa kupoteza muda.

Burkina Faso waliendelea kulinda lango lao dhidi ya mashambulizi ya Tunisia yaliyokuwa yakiongezeka na kumaliza mchezo huo kwa ushindi wa bao 1-0.

Safari ya Tunisia imefika mwisho ambao walikuwa wakitazamia kurudia kile walichokifanya kwenye AFCON 2004, walipokuwa mabingwa.

Burkina Faso Stallions wameweka historia nchini kwao kufika tena hatua hii ya nusu fainali ambapo itakumbukwa walitinga katika fainali mwaka 2013, na kufungwa 1-0 na Nigeria, na miaka miwili baadaye waliishia katika awamu ya makundi na kisha mwaka 2017 wakapoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya Misri katika nusu fainali.

Hawakuweza kufuzu mwaka 2019 lakini wamerejea kwa kishindo katika mashindano ya mwaka huu.

XS
SM
MD
LG